MKAGUZI DARAJA LA II

NAOT_Nafasi_121

MKAGUZI DARAJA LA II – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT)

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) imetangaza ajira mpya kwa nafasi ya MKAGUZI DARAJA LA II zenye jumla ya nafasi 121. Hii ni fursa muhimu kwa wahitimu wa uhasibu na fedha wanaotamani kufanya kazi serikalini.


📌 Taarifa za Kazi

  • TaasisI: Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT)
  • Cheo: Mkaguzi Daraja la II
  • Idadi ya Nafasi: 121
  • Ngazi ya Mshahara: SAIS. E
  • Kipindi cha Maombi: 10/01/2026 – 24/01/2026

📝 Majukumu ya Kazi

  • Kushiriki katika kuandaa na kutekeleza mpango wa ukaguzi (audit programme)
  • Kuandaa taarifa za kila robo mwaka na kuziwasilisha kwa msimamizi wa kazi
  • Kukagua hati za malipo, stakabadhi na akaunti za benki
  • Kufanya uchunguzi wa mifumo ya udhibiti wa ndani na kuandaa hoja za ukaguzi
  • Kufanya ukaguzi wa kushtukiza wa fedha
  • Kutekeleza mwongozo wa ukaguzi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
  • Kushirikiana na wakaguliwa kujadili masuala ya maendeleo ya ukaguzi
  • Kukagua matumizi, maendeleo, amana, wakala, miradi maalum na mapato ya Serikali
  • Kutayarisha barua, hoja na taarifa za ukaguzi za kila mwaka
  • Kufanya kazi nyingine zitakazopangiwa kulingana na fani yake

🎓 Sifa za Mwombaji

Waombaji wanapaswa kuwa na mojawapo ya sifa zifuatazo:

  • Shahada ya Kwanza ya Biashara au Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu
  • Bachelor of Accounting with Information Technology
  • Bachelor of Accounting and Finance
  • Bachelor in Public Sector Accounting and Finance

Vyeti vinapaswa kuwa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.


💼 Mshahara

Mshahara utalipwa kulingana na ngazi ya SAIS. E kwa mujibu wa utaratibu wa Serikali.


🖥️ Jinsi ya Kuomba

Waombaji wote wanatakiwa kuomba kazi kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal.

Tarehe ya mwisho ya kuomba: 24 Januari 2026


📢 Pata Taarifa Zaidi za Ajira

Jiunge na channel yetu ya WhatsApp kwa ajira za Serikali, sekta binafsi, maandalizi ya usaili na fursa za uhasibu na biashara.

Kwa maoni au ushirikiano wa kibiashara: business@vedastuswatosha.sbs