Nafasi za Kazi ATCL SACCOS LTD – Dar es Salaam 2026

job_vaccancy

Nafasi za Kazi ATCL SACCOS LTD – Januari 2026

ATCL SACCOS LTD ni chama cha ushirika wa kifedha (Savings and Credit Cooperative Society) kilichoanzishwa Novemba 2021 kwa lengo la kuwawezesha wanachama wake kiuchumi kupitia huduma za akiba, hisa na mikopo.

Kwa sasa, ATCL SACCOS LTD kinatangaza nafasi 3 za kazi na mafunzo (internship) kwa waombaji wenye sifa stahiki kufanya kazi Dar es Salaam.


📌 Taarifa za Jumla

  • Taasis: ATCL SACCOS LTD
  • Eneo: Dar es Salaam
  • Tarehe ya Kutangazwa: 18 Januari 2026
  • Aina ya Ajira: Full-time
  • Mshahara: Kivutio kulingana na sera za ATCL SACCOS LTD
  • Deadline: 7 Februari 2026

🧾 Nafasi Zilizopo

1️⃣ Loan Officer (Nafasi 1)

Lengo la Kazi: Kusimamia, kuchakata, kufuatilia na kurejesha mikopo kwa wanachama.

Sifa za Mwombaji:

  • Diploma au Shahada ya Uhasibu, Fedha, Uchumi, Biashara au Cooperative Management
  • Uzoefu wa angalau mwaka 1 katika usimamizi wa mikopo (faida zaidi)
  • Uelewa wa mifumo ya SACCOS ni faida
  • Umri: Miaka 20 – 40

Majukumu:

  • Kupokea na kuchambua maombi ya mikopo
  • Kufanya uhakiki wa wanachama
  • Kufuatilia marejesho ya mikopo
  • Kushughulikia mikopo chechefu na urejeshaji
  • Kutoa elimu ya mikopo kwa wanachama

2️⃣ Assistant Accountant (Nafasi 1)

Lengo la Kazi: Kusimamia malipo, mapato, mali na kumbukumbu za kifedha.

Sifa za Mwombaji:

  • Shahada ya Uhasibu, Fedha au inayofanana
  • Uzoefu wa angalau mwaka 1 kwenye kazi za uhasibu
  • Uwezo wa kutumia accounting software
  • Umri: Miaka 20 – 40

Majukumu:

  • Kufanya bank reconciliation za kila mwezi
  • Kuingiza invoices, vouchers na petty cash kwenye mfumo
  • Kuandaa taarifa za matumizi ya kila mwezi
  • Kusimamia malipo ya EFT
  • Kuhakikisha matumizi yanazingatia bajeti

3️⃣ ICT Intern (Nafasi 1)

Lengo la Mafunzo: Kusaidia shughuli za kila siku za ICT huku ukipata uzoefu wa vitendo.

Sifa:

  • Diploma au Shahada ya IT, Computer Science au Information Systems
  • Mhitimu mpya au mwanafunzi wa industrial training
  • Uelewa wa msingi wa networking na databases
  • Umri: Miaka 20 – 30

Majukumu:

  • Kutoa msaada wa vifaa na mifumo ya TEHAMA
  • Kusaidia matengenezo ya mifumo
  • Kusaidia data entry, backups na updates
  • Kusimamia vifaa vya ICT

📨 Namna ya Kutuma Maombi

Nyaraka Zinazohitajika:

  • Barua ya maombi iliyoandikwa vizuri
  • CV iliyosasishwa
  • Picha moja (passport size)
  • Vyeti vya masomo na taaluma vilivyothibitishwa

Maombi yawasilishwe kwa nakala ya karatasi (hard copy) na nakala ya mtandaoni (soft copy).

Anuani ya Posta:
The Chairperson,
ATCL SACCOS LTD,
P.O. Box 543,
Dar es Salaam

Email: customer.care@atclsaccos.co.tz

Deadline: 7 Februari 2026


📢 Kwa job alerts zaidi, maandalizi ya usaili na mock tests:
Fuata USAILI PORTAL WhatsApp Channel: